Jump to content

Legal:Wikimania 2025 Evaluation Survey Privacy Statement/sw

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
This page is a translated version of the page Legal:Wikimania 2025 Evaluation Survey Privacy Statement and the translation is 33% complete.

Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Wikimania 2025 Evaluation Survey. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.

Muhtasari wa Taarifa ya Faragha
Wikimania 2025 Evaluation Survey
Kutoka Timu ya Mawasiliano ya Harakati
illustration
Data tunayokusanya itatumika kwa uchanganuzi na utafiti wa wazi
Data Iliyokusanywa
MajibuNdiyo
Data ya demografiaNdiyo
KurekodiHapana
Data iliyochapishwa
YasiyotambulishaNdiyo
YanayotambulishaHapana
Ufikiaji wa Data
Wikimedia FoundationNdiyo
WanaojitoleaHapana
Watoa huduma
  • LimeSurvey
Hifadhi ya Data na Ufutaji
Uzuiaji wa Data GhafiSiku 180
Eneo la DataMarekani na maeneo mengine
Tafadhali soma Taarifa kamili ya Faragha


ikoni Kukusanya na Kutumia Maelezo

Sababu ya kukusanya maelezo yako

Mradi huu utatusaidia kuongeza uendelevu wa harakati yetu, tathimini, thibitisha na zoea na uratibu kwa wadau wote. Tutatumia maelezo unayotupa:

  • Kuendesha tukio au mkutano husika

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali soma ukurasa wake husika.

Jinsi tunavyokusanya maelezo yako

LimeSurvey hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.

Maelezo tunayokusanya

Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.

Majibu ya maswali
kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
Maelezo ya demografia
kama vile utaifa, jinsia

ikoni Kushiriki

Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako

Kuchapisha: Tutachapisha tu data isiyotambua (kama vile manukuu, takwimu zisizo na majina au data nyingine ya jumla). Kwa mfano, tafadhali kagua kile ambacho tulichapisha awali. Ili kuwezesha uchapishaji huu, unakubali kuchangia michango yako yenye hakibunifu kwa kikoa cha umma chini ya masharti ya Creative Commons Zero 1.0.

Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.

Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.

ikoni Ulinzi

Muda ambao tunahifadhi maelezo yako

Data tunayokusanya itafutwa, kutolewa utambulisho, au kujumlishwa ndani ya siku 180. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.

Mtu wa kuwasiliana naye

Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa wikimania@wikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.


Tafadhali kumbuka kuwa ikitokea tofauti yoyote ya maana au ufafanuzi kati ya toleo asili la Kiingereza na tafsiri ya Taarifa hii ya Faragha, toleo asili la Kiingereza linachukua nafasi ya kwanza.