Jump to content

Sera:Sera ya Ufikiaji wa Wikimedia kwa Anwani za IP za Akaunti ya Muda

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
This page is a translated version of the page Policy:Wikimedia Access to Temporary Account IP Addresses Policy and the translation is 88% complete.
Outdated translations are marked like this.

Ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda huwasaidia watumiaji kulinda miradi ya Wikimedia. Ufikiaji huu ni tofauti na ufikiaji wa zana ya Habari ya IP. Kama sharti la ufikiaji, watumiaji ambao hawajakubali Ufikiaji wa sera ya data ya kibinafsi isiyo ya umma lazima wakubali miongozo ifuatayo.

Background

Miradi ya Wikimedia ni bidhaa shirikishi ya jumuiya ya kimataifa ya watumiaji wa kujitolea. Miradi inaweza kuhaririwa na au bila kuingia katika akaunti ya Wikimedia. Wale wanaohariri bila kuingia katika akaunti ya Wikimedia hufanya hivyo kwa kutumia akaunti ya muda, ambayo haina sifa za kuingia.

Purpose

Shirika la Wikimedia Foundation huwapa watumiaji fulani walioingia katika akaunti ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda ili kuwawezesha watumiaji hawa kutekeleza au kuchunguza ukiukaji unaoweza kutokea kwa Shirika la Wikimedia Foundation au sera za watumiaji za jumuiya. Ufikiaji hutumiwa kupambana na uharibifu na barua taka, kuangalia matumizi mabaya ya akauntibandia, na kupunguza usumbufu kwa miradi ya Wikimedia.

Matumizi na ufichuzi wa anwani za IP za akaunti za muda

Kuingia kwenye anwani za IP za wahariri waliotoka umezuiwa na sera. Hii inahakikisha kwamba taarifa inatumika tu kwa utendakazi wa kupinga unyanyasaji kwenye miradi ya Wikimedia. Watumiaji wenye ufikiaji wa anwani za IP hawapaswi kuzitoa kwa mtu ambaye hana ruhusa sawa za kuingia isipokuwa ufichuzi unaruhusiwa kulingana na mwongozo ulio hapa chini.

Wahusika wa nje ambao wanaweza kutaka kufikia anwani za IP wanaweza kuwasiliana na watumiaji ambao wana haki hii kwa kujaribu kupata taarifa hiyo. Watumiaji walio na haki za ufikiaji wa IP wanapaswa kufahamu hili, na kuwa macho juu ya uwezekano wa maombi ya ufikiaji wa kutiliwa shaka.

Matumizi ya anwani za IP za akaunti za muda

Matumizi ya anwani za IP za akaunti za muda ni kwa ajili ya uchunguzi tu wa au kutekeleza sheria dhidi ya uharibifu, matumizi mabaya, barua taka, unyanyasaji, tabia ya usumbufu na ukiukaji mwingine wa sera za jumuiya au Shirika la Wikimedia Foundation. Ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda unapaswa kuwa kwa misingi inayohitajika na kwa kufuata miongozo hii, Sera ya Faragha na sera za ndani zenye vizuizi zaidi zinazotumika kwa mradi husika.

Ufikiaji haupaswi kutumiwa katika udhibiti wa kisiasa, kutumia shinikizo kwa wahariri, au kama tishio dhidi ya mhariri mwingine katika mzozo wa maudhui. Lazima kuwe na sababu halali ya kuchunguza mtumiaji wa muda. Kumbuka kuwa kutumia akaunti nyingi za muda kunaruhusiwa, mradi hazitumiki katika ukiukaji wa sera (mfano wa ukiukaji ni pamoja na kukwepa vizuizi au marufuku).

Wale walio na ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda wana uwezo wa kubainisha ni kutoka anwani za IP zipi ambazo akaunti ya muda imefanya mabadiliko au vitendo vya kuingia kwenye Wikimedia wiki. Taarifa hii inahifadhiwa kwa muda mfupi tu (kwa sasa ni siku 90), kwa hivyo anwani za IP zilizotumiwa kabla ya hapo hazitaonyeshwa. Anwani za IP zinapatikana kwa kubofya "Onyesha IP" kwenye kumbukumbu, historia, na kurasa za mabadiliko ya hivi karibuni. Anwani za IP zinapatikana pia kupitia zana ya Taarifa ya IP.

Vitendo vifuatavyo vinarekodiwa:

  • Mtumiaji anapokubali upendeleo ambao uwezesha au kutowezesha ufunuo wa IP kwa akaunti yake.
  • Kufichua anwani ya IP ya akaunti ya muda.
  • Kuorodhesha akaunti za muda ambazo zinahusishwa na anwani ya IP.

Ufichuzi

Hata kama mtumiaji anakiuka sera, epuka kufichua taarifa ya kibinafsi ikiwezekana. Tumia majina ya watumiaji ya akaunti ya muda badala ya kufichua anwani za IP moja kwa moja, au toa taarifa kama vile mtandao sawa/si mtandao sawa au wa kufanana.

Wakati wa kuweka miradi na watumiaji wengine salama, watumiaji bado wanaweza kuhitaji kufichua anwani za IP za akaunti za muda kwa wahusika wengine. Ufichuzi unaoruhusiwa ni mdogo kwa hali zifuatazo:

  • Watumiaji walio na ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda wanaweza kufichua anwani za IP kwa faragha kwa watumiaji wengine ambao wana haki sawa za ufikiaji.
  • Inapoaminika kuwa ni muhimu, watumiaji walio na ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda wanaweza pia kufichua anwani za IP katika maeneo yanayofaa ambayo yanawawezesha kutekeleza au kuchunguza ukiukaji unaoweza kutokea wa Sheria na Masharti yetu, Sera ya Faragha, au sera zozote za Shirika la Wikimedia Foundation au za watumiaji wa jumuiya. Maeneo yanayofaa ya ufichuzi kama huo ni pamoja na kurasa zilizowekwa kwa Matumizi mabaya ya muda mrefu. Ikiwa ufichuzi kama huo baadaye hauhitajiki, basi anwani ya IP inapaswa kufutwa mara moja.
  • Watumiaji ambao wamekubali sera tofauti ya Ufikiaji wa data ya kibinafsi isiyo ya umma wanaweza pia kufichua anwani za IP za akaunti za muda kama inavyoruhusiwa chini ya sera hiyo.

Ikiwa anwani za IP za akaunti za muda zinahitaji kufichuliwa kuhusiana na tishio linalokaribia madhara ya kimwili, mara moja tuma barua pepe emergency@wikimedia.org na maelezo ya ombi ili liweze kutathminiwa kwa uwezekano wa ufichuzi wa Shirika.

Watumiaji wanaweza kuripoti maombi yoyote rasmi na yasiyo rasmi wanayopokea ambayo hayako chini ya upeo ulioidhinishwa wa sera hii, ikijumuisha wito kutoka kwa watekelezaji sheria, mawakala wa serikali, mawakili, au wahusika wengine, kwa idara ya sheria ya Shirika la Wikimedia Foundation kwenye legal@wikimedia.org.

Mahitaji ya chini kabisa ya ufikiaji

Ufikiaji unapatikana kwa watumiaji walioingia tu. Ili kupata ufikiaji, watumiaji lazima watimize mahitaji yanayotumika kwa kikundi chao cha watumiaji, ambayo yameorodheshwa hapa chini. Watumiaji wanaohitimu ufikiaji wa kimataifa na ufikiaji wa ndani, wanahitaji tu kukidhi mahitaji yanayohusiana na ufikiaji wa kimataifa.

Ufikiaji wa kimataifa

Washiriki wa vikundi fulani vya watumiaji wa kimataifa na vikundi fulani vya watumiaji wa ndani wanahitaji ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda kwenye miradi yote ya Wikimedia ili kutekeleza majukumu yao. Mahitaji ya ufikiaji hutegemea kikundi cha watumiaji. Watumiaji ambao ni wanachama wa zaidi ya moja ya vikundi vya watumiaji vilivyo hapa chini wanahitaji tu kutimiza mahitaji ya mojawapo ya vikundi vyao vya watumiaji. Kwa mfano, mwanachama wa vikundi vya watumiaji vya Wachunguzi Maalum na wadumishaji wa Kichujio cha matumizi mabaya watapata ufikiaji wa kiotomatiki kupitia mahitaji ya Wachunguzi Maalum; ufikiaji wa mtumiaji kama huyo bado ungekuwa wa majukumu yote mawili.

Wasimamizi, Wachunguzi Maalum, U4C, na Wafanyakazi

Ufikiaji hutolewa kiotomatiki kwa watumiaji ambao ni wanachama wa mojawapo ya vikundi vya watumiaji vifuatavyo duniani: Wasimamizi, Wachunguzi Maalum, Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) na Wafanyakazi. Wasimamizi, Wachunguzi Maalum, na wanachama wa U4C wanatarajiwa kushughulikia anwani za IP kulingana na miongozo hii na sera ya Ufikiaji wa data isiyo ya umma. Wafanyikazi wanatarajiwa kushughulikia anwani za IP kulingana na NDA yao.

Wasimamizi wa kimataifa, Warudisha nyuma mabadiliko wa kimataifa, na Watunzaji vichujio vya matumizi mabaya na wasaidizi

Wanachama wa vikundi vya watumiaji vya Wasimamizi ya kimataifa, Warudisha nyuma mabadiliko wa kimataifa, Watunzaji vichujio vya matumizi mabaya, na Wasaidizi wa vichujio vya matumizi mabaya wanaweza kujijumuisha kote ulimwenguni kupitia Special:GlobalPreferences. Watumiaji hawa lazima wakubali kutumia anwani za IP kwa mujibu wa miongozo hii, kwa ajili ya uchunguzi au kuzuia tu uharibifu, matumizi mabaya au ukiukaji mwingine wa Shirika la Wikimedia Foundation au sera za jumuiya. Vinginevyo, watumiaji hawa wanaweza kuchagua kutojijumuisha kimataifa; ufikiaji wa kimataifa basi hautatolewa mradi tu watumiaji sio washiriki wa vikundi vya watumiaji ulimwenguni ambavyo vina ufikiaji wa kiotomatiki.

WatumiajiwaCheki na Waangalizi

Watumiaji ambao ni wanachama wa vikundi vya ndani vya WatumiajiwaCheki au Waangalizi wanaweza kujijumuisha kote ulimwenguni kupitia Special:GlobalPreferences. Watumiaji hawa wanatarajiwa kuchukulia anwani za IP kulingana na miongozo hii na sera ya Ufikiaji wa data isiyo ya umma.

Ufikiaji wa ndani

Baadhi ya watumiaji wanahitaji ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda kwenye miradi ya Wikimedia ya "ndani" ili kulinda miradi hiyo. Mahitaji ya ufikiaji hutegemea kikundi cha watumiaji wa ndani. Watumiaji ambao ni wanachama wa zaidi ya moja ya vikundi vya watumiaji vilivyo hapa chini wanahitaji tu kutimiza mahitaji ya mojawapo ya vikundi vyao vya watumiaji. Kwa mfano, mwanachama wa vikundi vya ndani vya watumiaji vya WatumiajiwaCheki na Warasimu atapokea ufikiaji wa kiotomatiki kupitia mahitaji ya WatumiajiwaCheki; ufikiaji wa mtumiaji kama huyo bado ungekuwa wa majukumu yote mawili.

WatumiajiwaCheki na Waangalizi

Ufikiaji wa ndani unatolewa kiotomatiki kwa watumiaji ambao ni wanachama wa vikundi vya watumiaji vya WatumiajiwaCheki au Waangalizi. Watumiaji hawa wanatarajiwa kuzichukulia anwani za IP kulingana na miongozo hii na sera ya Ufikiaji wa data isiyo ya umma.

Wasimamizi na Warasimu

Wasimamizi wa ndani na Warasimu wanaweza kuchagua kuingia kupitia Special:Preferences kwenye mradi wa ndani na kukubali kutumia anwani za IP kwa mujibu wa miongozo hii, kwa uchunguzi tu au kuzuia uharibifu, matumizi mabaya au ukiukaji mwingine wa Shirika la Wikimedia Foundation au sera za jumuiya. Vinginevyo, watumiaji hawa wanaweza kuchagua kutojijumuisha; basi ufikiaji hautatolewa mradi tu watumiaji si wanachama wa vikundi vya watumiaji ambavyo vina ufikiaji wa kiotomatiki.

Watumiaji wengine

Watumiaji ambao si mwanachama wa mojawapo ya vikundi vilivyo hapo juu hata hivyo wanaweza kuhitaji kufikia anwani za IP za akaunti za muda ili kusaidia katika doria, uchunguzi wa akaunti bandia, au kazi nyinginezo ili kulinda miradi ya Wikimedia.

Ili kufikia anwani za IP za akaunti za muda, watumiaji hawa lazima:

  1. Kukidhi mahitaji yote ya jumla yafuatayo:
    1. Akaunti ya mtumiaji ina umri wa angalau miezi 6, na
    2. Akaunti ya mtumiaji imefanya hariri zisizopungua 300 kwa mradi wa ndani.
  2. Wawasilishe ombi la ufikiaji kwa wakabidhi wa ndani au Wasimamizi. Kunaweza kuwa na mahitaji ya ziada kama sehemu ya ukaguzi huu, kama vile:
    1. Kiwango cha chini cha hariri 600 katika ukurasa mkuu kwa miradi ya ndani
    2. Wameonyesha ushahidi wa kazi ya doria ya awali,
    3. Mchakato wa uchaguzi wa jumuiya, na/au
    4. Mahitaji mengine yoyote, mradi tu mahitaji sio chini kuliko mahitaji ya jumla.
  3. Wajijumuishe kupitia Maalum:Mapendekezo kwenye mradi wa ndani, na
  4. Wakubali kutumia anwani za IP kwa mujibu wa miongozo hii, kwa ajili ya uchunguzi tu au kuzuia uharibifu, matumizi mabaya au ukiukaji mwingine wa sera za Shirika la Wikimedia Foundation au jumuiya, na kuelewa hatari na majukumu yanayohusiana na fursa hii.

Ili kudumisha ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda, watumiaji katika kundi hili lazima wahariri au kufanya kitendo kilichorekodiwa kwenye mradi wa ndani angalau mara moja ndani ya kipindi cha siku 365.

Bighairi kwa mahitaji ya chini

Ikiwa akaunti ya mtumiaji haifikii vigezo vilivyo hapo juu, lakini bado ina sababu halali ya kufikia anwani za IP za akaunti za muda, kwa madhumuni ambayo hayawezi kushughulikiwa ipasavyo na watumiaji ambao tayari wana ufikiaji huu, Wasimamizi wameidhinishwa kutoa bighairi kwa vigezo vilivyo hapo juu.

Kuondoa ufikiaji

Watumiaji ambao wamepewa ufikiaji wenyewe wanaweza kuacha ufikiaji wao kwa hiari wakati wowote kwa kutembelea Maalum:Mapendekezo. Watumiaji ambao wamezuiwa kabisa kuhariri mradi wa Wikimedia watapoteza ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda kwenye mradi huo. Wanachama wa kikundi cha watumiaji walio na ufikiaji wa kiotomatiki ambao hawataki kuwa na upendeleo huu wa ufikiaji wanapaswa kuwasiliana na ca@wikimedia.org.

Wasimamizi wameidhinishwa kusitisha ufikiaji wa mtumiaji ikiwa mtumiaji amebainika kuwa ametumia vibaya anwani za IP za akaunti za muda au makubaliano ya jumuiya ya karibu yanaamuru kuondolewa. Maombi ya kuondoa au kurekebisha ufikiaji wa anwani za IP za akaunti za muda yanaweza kuletwa kwa msimamizi kwa kutuma ombi [[ca@wikimedia.org|Maombi/Ruhusa za Wasimamizi#Kuondolewa kwa ufikiaji]]. Wakati kuna maafikiano ya jumuiya kuhusu kubatilisha haki za ufikiaji za mtumiaji, kiungo cha mjadala lazima kitolewe.

Other users who have been given access manually may voluntarily give up their access at any time by visiting Special:Preferences. If a user given access manually is determined to have misused temporary account IP addresses, or local community consensus dictates removal, then the users authorized to grant such access are also authorized to terminate access.

Requests for stewards to remove or amend access to temporary account IP addresses may be placed on Steward requests/Permissions#Removal of access. When there is community consensus regarding revocation of a user's access rights, a link to the discussion must be provided.

Ikihitajika, maombi ya kukaguliwa na wafanyakazi wa Imani na Usalama yanaweza kufanywa kupitia ca@wikimedia.org,, na ufikiaji wa mtumiaji kuondolewa kwa mujibu wa sera ya vitendo vya Ofisi. Malalamiko kuhusu ukiukaji wa Sera ya Faragha yataendelezwa ili kukaguliwa na tume ya wachunguzi maalum.

Ili kuhakikisha uwajibikaji, kumbukumbu huwekwa ambayo watumiaji wanaweza kufikia anwani za IP za akaunti za muda.

Notes


See also