Legal:Community Insights 2024 Survey Privacy Statement/sw

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
This page is a translated version of the page Legal:Community Insights 2024 Survey Privacy Statement and the translation is 0% complete.

Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Community Insights 2024 Survey. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.

Muhtasari wa Taarifa ya Faragha
Community Insights 2024 Survey
Kutoka Research team
illustration
Data tunayokusanya itatumika kukagua au kuimarisha huduma zetu
Data Iliyokusanywa
MajibuNdiyo
Data ya demografiaNdiyo
KurekodiHapana
Data ya kifaaNdiyo
Data iliyochapishwa
YasiyotambulishaNdiyo
YanayotambulishaHapana
Ufikiaji wa Data
Wikimedia FoundationNdiyo
WanaojitoleaNdiyo
Watoa huduma
  • Qualtrics
Hifadhi ya Data na Ufutaji
Uzuiaji wa Data GhafiSiku 90
Eneo la DataMarekani na maeneo mengine
Tafadhali soma Taarifa kamili ya Faragha


ikoni Kukusanya na Kutumia Maelezo

Sababu ya kukusanya maelezo yako

Mradi huu utatusaidia kutoa usalama na ujumuishaji, kuongeza uendelevu wa harakati yetu na kuboresha mazingira ya mtumiaji. Tutatumia maelezo unayotupa:

  • Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
  • Kusaidia jitihada za ustawi wa jamii
  • Kukuza maarifa kupitia utafiti wa wazi

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali soma ukurasa wake husika.

Jinsi tunavyokusanya maelezo yako

Qualtrics hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.

Maelezo tunayokusanya

Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.

Majibu ya maswali
kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
Maelezo ya demografia
kama vile utaifa, jinsia
Pia tutakusanya yafuatayo kwa kutumia huduma zilizotambuliwa hapo juu:
Maelezo ya kifaa
kama vile anwani ya IP, ajenti ya mtumiaji

ikoni Kushiriki

Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako

Kuchapisha: Tutachapisha tu data isiyotambua (kama vile manukuu, takwimu zisizo na majina au data nyingine ya jumla). Kwa mfano, tafadhali kagua kile ambacho tulichapisha awali. To facilitate this publishing, you agree to donate your copyrightable contributions to the public domain under the terms of Creative Commons Zero 1.0.

Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji, watoa huduma na watu wanaojitolea wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.

Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.

ikoni Ulinzi

Muda ambao tunahifadhi maelezo yako

Data tunayokusanya itafutwa, kutolewa utambulisho, au kujumlishwa ndani ya siku 90. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.

Mtu wa kuwasiliana naye

Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa surveys@wikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.


Tafadhali kumbuka kuwa ikitokea tofauti yoyote ya maana au ufafanuzi kati ya toleo asili la Kiingereza na tafsiri ya Taarifa hii ya Faragha, toleo asili la Kiingereza linachukua nafasi ya kwanza.