Legal:Event Registration: Organizer Experiences Video Privacy Statement/sw

From Wikimedia Foundation Governance Wiki

Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Event Registration: Organizer Experiences Video. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.

Muhtasari wa Taarifa ya Faragha
Event Registration: Organizer Experiences Video
Kutoka Campaigns team
illustration
Data tunayokusanya itatumika kukagua au kuimarisha huduma zetu
Data Iliyokusanywa
MajibuNdiyo
Maelezo ya mawasilianoNdiyo
KurekodiNdiyo
HatiNdiyo
Data iliyochapishwa
YasiyotambulishaHapana
YanayotambulishaNdiyo
Ufikiaji wa Data
Wikimedia FoundationNdiyo
WanaojitoleaHapana
Watoa huduma
  • Google Forms
  • Google Meet
Hifadhi ya Data na Ufutaji
Uzuiaji wa Data GhafiMuda Usiobainika
Eneo la DataMarekani na maeneo mengine
Tafadhali soma Taarifa kamili ya Faragha


ikoni Kukusanya na Kutumia Maelezo

Sababu ya kukusanya maelezo yako

Mradi huu utatusaidia tathimini, thibitisha na zoea, kuwekeza katikamaendeleo ya ujuzi na uongozi na kuboresha mazingira ya mtumiaji. Tutatumia maelezo unayotupa:

  • Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
  • Kuwasiliana nawe zaidi

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali soma ukurasa wake husika.

Jinsi tunavyokusanya maelezo yako

Google Forms hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake. Google Meet hutumiwa pia kuandaa mkutano au kutiririsha tukio; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.

Maelezo tunayokusanya

Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.

Majibu ya maswali
kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
Maelezo ya mawasiliano
kama vile jina, jina la mtumiaji, anwani ya barua pepe
Pia tutakusanya yafuatayo kwa kutumia huduma zilizotambuliwa hapo juu:
Rekodi
kama vile video, sauti, picha
Hati
kama vile rekodi za gumzo, manukuu, picha za skrini

ikoni Kushiriki

Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako

Kuchapisha: Tutachapisha data ya kutambua (kama vile manukuu ya moja kwa moja pamoja na sifa). Ili kuwezesha uchapishaji huu, unakubali kuchangia michango yako yenye hakibunifu kwa kikoa cha umma chini ya masharti ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 na 4.0.

Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.

Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.

ikoni Ulinzi

Muda ambao tunahifadhi maelezo yako

Data ghafi tunayokusanya inaweza kuhifadhiwa kwa muda usiobainika. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.

Mtu wa kuwasiliana naye

Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa ifried@wikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.


Tafadhali kumbuka kuwa ikitokea tofauti yoyote ya maana au ufafanuzi kati ya toleo asili la Kiingereza na tafsiri ya Taarifa hii ya Faragha, toleo asili la Kiingereza linachukua nafasi ya kwanza.