Legal:Journey Transitions Privacy Statement/sw
Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Journey Transitions. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.
Kukusanya na Kutumia Maelezo
Sababu ya kukusanya maelezo yako
Mradi huu utatusaidia kuongeza uendelevu wa harakati yetu, kutambua mada zenye tija na tathimini, thibitisha na zoea. Tutatumia maelezo unayotupa:
- Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
- Kupata wanaotuma maombi, washiriki au teuzi
- Kuwasiliana nawe zaidi
- Kukuza maarifa kupitia utafiti wa wazi
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali tuma barua pepe kwa dchenwikimedia.org.
Jinsi tunavyokusanya maelezo yako
QuickSurveys hutumiwa kukusanya majibu ya utafiti; tafadhali soma kurasa zake kwenye Meta-Wiki na MediaWiki. Ili kutusaidia kuelewa vipi na kwa nini watumiaji wetu hutembelea miradi ya Wikimedia, tutaunganisha majibu yako ya utafiti kwenye data ya ziada ambayo QuickSurveys hukusanya, ambayo imeelezwa hapa chini. Google Forms hutumiwa pia kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake. Google Meet hutumiwa pia kuandaa mkutano au kutiririsha tukio; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.
Maelezo tunayokusanya
Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.
Majibu ya maswali
- kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
Maelezo ya mawasiliano
- kama vile jina, jina la mtumiaji, anwani ya barua pepe
Maelezo ya demografia
- kama vile utaifa, jinsia
Rekodi
- kama vile video, sauti, picha
Maelezo ya kifaa
- kama vile anwani ya IP, ajenti ya mtumiaji
Maelezo yasiyo ya umma ya kipindi cha Wikimedia
- kama vile ukurasa uliotazamwa, hali ya kuingia
Kushiriki
Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako
Kuchapisha: Tutachapisha tu data isiyotambua (kama vile manukuu, takwimu zisizo na majina au data nyingine ya jumla). Ili kuwezesha uchapishaji huu, unakubali kuchangia michango yako yenye hakibunifu kwa kikoa cha umma chini ya masharti ya Creative Commons Zero 1.0.
Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua. Tafadhali fahamu kwamba tunashirikiana na an external research vendor, ambaye pia anabanwa na majukumu ya mkataba kuzingatia maelezo yako mara kwa mara kwa kanuni za Sera yetu ya Faragha.
Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.
Ulinzi
Muda ambao tunahifadhi maelezo yako
Data tunayokusanya itafutwa, kutolewa utambulisho, au kujumlishwa ndani ya siku 90. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.
Mtu wa kuwasiliana naye
Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa dchenwikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.