Legal:Wikimania 2025 Travel Scholarship Privacy Statement/sw
Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Wikimania 2025 Travel Scholarship. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.
Kukusanya na Kutumia Maelezo
Sababu ya kukusanya maelezo yako
Mradi huu utatusaidia kuongeza uendelevu wa harakati yetu, uratibu kwa wadau wote na kuwekeza katikamaendeleo ya ujuzi na uongozi. Tutatumia maelezo unayotupa:
- Kupata wanaotuma maombi, washiriki au teuzi
- Kuwasiliana nawe zaidi
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali tuma barua pepe kwa wikimaniawikimedia.org.
Jinsi tunavyokusanya maelezo yako
LimeSurvey hutumiwa kukusanya majibu au usajili; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake.
Maelezo tunayokusanya
Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.
- Majibu ya maswali
- kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
- Maelezo ya mawasiliano
- kama vile jina, jina la mtumiaji, anwani ya barua pepe
- Maelezo ya demografia
- kama vile utaifa, jinsia
- Maelezo ya umma ya shughuli ya Wikimedia
- kama vile michango ya watumiaji au rekodi za umma
Kushiriki
Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako
Kuchapisha: Tutachapisha tu data isiyotambua (kama vile manukuu, takwimu zisizo na majina au data nyingine ya jumla). To facilitate this publishing, you agree to donate your copyrightable contributions to the public domain under the terms of Creative Commons Zero 1.0.
Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji, watoa huduma na watu wanaojitolea wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.
Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.
Ulinzi
Muda ambao tunahifadhi maelezo yako
Data tunayokusanya itafutwa, kutolewa utambulisho, au kujumlishwa ndani ya siku 90. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.
Mtu wa kuwasiliana naye
Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa wikimaniawikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.