Legal:Language Community Meetings Privacy Statement/sw
Taarifa hii ya faragha inatimiliza Sera ya Faragha ya Wikimedia Foundation ya washiriki Language Community Meetings. Tunaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kushiriki, kuhifadhi na kufuta maelezo tunayopokea kutoka kwa washiriki.
Kukusanya na Kutumia Maelezo
Sababu ya kukusanya maelezo yako
Mradi huu utatusaidia kuwekeza katikamaendeleo ya ujuzi na uongozi, kuhakikisha usawa katika kufanya maamuzi na kuongeza uendelevu wa harakati yetu. Tutatumia maelezo unayotupa:
- Kuendesha tukio au mkutano husika
- Kuimarisha miradi, zana na huduma zetu
- Kupata wanaotuma maombi, washiriki au teuzi
- Kusaidia jitihada za ustawi wa jamii
- Kuwasiliana nawe zaidi
- Kukuza maarifa kupitia utafiti wa wazi
Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu, tafadhali soma ukurasa wake husika.
Jinsi tunavyokusanya maelezo yako
Google Meet hutumiwa kuandaa mkutano au kutiririsha tukio; tafadhali soma Sera ya Faragha na Sheria ya Masharti yake. Notes will be taken on Etherpad .
Maelezo tunayokusanya
Ukichagua kushiriki, tutakuomba utoe aina zifuatazo za maelezo.
- Majibu ya maswali
- kama vile majibu yaliyofafanuliwa na huru
- Maelezo ya mawasiliano
- kama vile jina, jina la mtumiaji, anwani ya barua pepe
- Mawasilisho ya midia
- kama vile video, picha, slaidi
- Rekodi
- kama vile video, sauti, picha
- Hati
- kama vile rekodi za gumzo, manukuu, picha za skrini
Kushiriki
Jinsi tunavyoshiriki maelezo yako
Kuchapisha: Tutachapisha data ya kutambua (kama vile manukuu ya moja kwa moja pamoja na sifa). Ili kuwezesha uchapishaji huu, unakubali kuchangia michango yako yenye hakibunifu kwa kikoa cha umma chini ya masharti ya Creative Commons Zero 1.0.
Ufikiaji: Data ghafi itashirikiwa tu na wafanyakazi wa Wikimedia, wachangiaji na watoa huduma wanaohitaji kuchakata maelezo haya na wanatii majukumu ya kutofichua.
Kushiriki kwingine: Huenda tukafichua maelezo yoyote tuliyokusanya inapohitajika kisheria, wakati tuna ruhusa yako, inapohitajika ili kulinda haki, faragha, usalama wako, watumiaji au umma kwa jumla na inapohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yetu au sera nyingine yoyote ya Wikimedia.
Ulinzi
Muda ambao tunahifadhi maelezo yako
Data ghafi tunayokusanya inaweza kuhifadhiwa kwa muda usiobainika. Tazama miongozo yetu ya uzuiaji wa data kwa maelezo zaidi.
Mtu wa kuwasiliana naye
Ikiwa una maswali, tafadhali tuma barua pepe kwa ssethiwikimedia.org. Washiriki ambao wangependa kubadilisha, kufikia au kufuta maelezo waliyotoa wanapaswa kuwasiliana nasi kwa maombi yao.