Jump to content

Resolution: Miongozo ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
This page is a translated version of the page Resolution:Approval of Universal Code of Conduct Enforcement Guidelines and the translation is 92% complete.
Resolutions Miongozo ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili Feedback?
Azimio hili lilipitishwa mnamo 9 Machi 2020.

Kwa kuwa, mnamo 2020, Bodi ya Wadhamini ilipitisha Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili ("UCoC") kama sera ya kubana kwenye miradi yote ya Wikimedia;

Kwa kuwa, awamu ijayo ya kutekeleza UCoC ni kutangaza miongozo ya utekelezaji;

Kwa kuwa, uchaguzi ulifanywa na jumuiya kuhusu kukubali rasimu ya kwanza ya miongozo ya utekelezaji wa UCoC mnamo Machi 2022;

Kwa kuwa, ingawa miongozo ya utekelezaji ilikubaliwa na asilimia 57 ya kura, kikoa cha mradi wa UCoC na Bodi ya Wadhamini zilifunga kurekebisha miongozo kwa kufuatana na shauri la jumuiya, na kufanya uchaguzi wa ziada;

Kwa kuwa, baada ya Machi 2022, Kamati ya Marekebisho yenye watu wajitoao na wafanyakazi walitayarisha marekebisho ya miongozo ya utekelezaji; na

Kwa kuwa, katika uchaguzi wa baadaye uliofanywa mnamo Januari hadi Februari 2023, miongozo ya utekelezaji kama ilivyorekebishwa ilipata kibali cha asilimia 76 ya wapiga kura;

Sasa, kwa hivyo,

IMEAZIMIWA, kwamba Bodi tangu sasa imepitisha Miongozo ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili kama ilivyorekebishwa.

Connect
Nataliia Tymkiv (Chair), Esra'a Al Shafei (Vice Chair), Shani Evenstein Sigalov (Vice Chair), Luis Bitenourt-Emilio, Victoria Doronina, Dariusz Jemielniak, Lorenzo Losa, Raju Narisetti, Mike Peel, Rosie Stephenson-Goodknight, Jimmy Wales
Wasiopo
Tanya Capuano

References