Maelezo zaidi kuhusu vipengele ambavyo havishughulikiwi na Sera hii ya Faragha
Hii ni sehemu ya Sera ya Faragha na inanuiwa kueleza kwa undani hali ambazo hazishughulikiwi na Sera yetu ya Faragha.
Tovuti za Wikimedia na Zana zilizo na sera mbadala
Tovuti au zana fulani za Wakfu wa Wikimedia zina sera mbadala za faragha au vifungu ambavyo vinatofautiana na Sera hii ya Faragha. Tovuti hizi zinajumuisha:
Duka la Wikimedia (linaloshughulikiwa chini ya sera ya duka);
donate.wikimedia.org, ikijumuisha mchakato wa kutoa ufadhili, kama vile kubofya kwenye bango la kutoa ufadhili (chini ya Sera ya Faragha ya Wafadhili); ya
Ikiwa tovuti ya Wakfu wa Wikimedia inadhibitiwa na sera mbadala ya faragha, itaunganishwa na sera hiyo. Wakati zana ya Wakfu wa Wikimedia kinatawaliwa na sera mbadala ya faragha, ukurasa ambao zana inaweza kupakuliwa au kuwezeshwa utajumuisha kiungo cha sera hiyo.
Wanajamii
Tovuti za Wikimedia ni kazi za kushirikiana kwa upendo ambazo zinaendelezwa na kusasishwa kila wakati na jamii ya watu wa kujitolea wa kutoka kote ulimwenguni. Jamii hii ya watu wa kujitolea wa kutoka kote ulimwenguni wakati mwingine inaweza kufikia maelezo ya kibinafsi ili kuhakikisha utendaji wa Tovuti za Wikimedia.
Wasimamizi wa kujitolea, kama vile CheckUsers au Watumishi. Hawa ni wasimamizi wa kujitolea wanaotekeleza sera za Tovuti za Wikimedia na kuhakikisha usalama wa Tovuti za Wikimedia. Wasimamizi hawa wakifikia Maelezo ya Kibinafsi yasiyo ya hadharani, wanatakiwa kutii Sera ya Ufikiaji wa Sera ya Maelezo yasiyo ya Hadharani, na sera zingine maalum za zana.
Watoa zana. Tunawezesha mifumo ya wasanidi programu wengine wa kujaribu na kusanidi zana na tovuti mpya, kama vile wmflabs.org. Unapotumia mojawapo ya zana zilizotengenezwa na watu hawa wa kujitolea, huenda utawahamishia maelezo. Watu hawa wa kujitolea wanapofikia maelezo yasiyo ya hadharani au Maelezo ya Kibinafsi, wanahitajika kutii masharti yanayodhibiti mfumo fulani unaoendesha zana hii.
Watumiaji wengine. Tunatoa zana kadhaa ambazo huwawezesha watumiaji kuwasiliana. Mawasiliano yanaweza kushughulikiwa na Sera hii yanapopitia katika mifumo yetu, lakini watumiaji wanaopokea mawasiliano haya, na kile wanachofanyia mawasiliano haya wanapoyapokea, ni mambo ambayo hayajashughulikiwa na Sera hii. Mifano inajumuisha:
kutuma ujumbe kwenye orodha za barua pepe zilizopangishwa na Wakfu;
kuomba usaidizi kwa watu wa kujitolea tukitumia mfumo wa mtandaoni wa kutoa tiketi (barua pepe zinazotumwa kwenye infowikimedia.org huenda kwenye mfumo huu);
kuwatumia barua pepe watumiaji wengine kupitia Tovuti za Wikimedia (kwa mfano, kwa kutumia huduma ya "Mtumie barua pepe mtumiaji huyu"); na
Kupiga gumzo kwenye IRC (kama vile kwenye kituo cha #wikipedia).
Watu wengine
Sera hii ya Faragha inashughulikia tu jinsi ambavyo Wakfu wa Wakfu wa Wikimedia anavyokusanya, kutumia na kufichua Maelezo ya Kibinafsi na haishughulikii kanuni za watu wengine. Kwa mfano, Sera hii ya Faragha haizungumzii kanuni za:
Tovuti zinazoendeshwa na mashirika mengine, kama vile tovuti zilizounganishwa kutoka sehemu za "Marejeleo" ya Wikipedia, au zinazoendeshwa na sura za Wikimedia au mashirika ya harakati. Mashirika haya yanaweza kupokea maelezo kutoka kwako ikiwa unatembelea tovuti zao baada ya kutumia mojawapo ya Tovuti za Wikimedia. Yanadhibitiwa na sera zao za faragha.
Programu za simu zinazotolewa na mashirika mengine au watu binafsi. Mashirika haya au watu binafsi wanaweza kupokea maelezo kutoka kwako ikiwa utatumia programu hizo kufikia Tovuti za Wikimedia au maudhui ya Tovuti za Wikimedia. Yanadhibitiwa na sera zao za faragha.
Wakati mwingine, watu wa kujitolea wanaweza kuweka zana ya kukusanya maelezo, kama vile hati, kifaa, pikseli ya ufuatiliaji au kitufe cha kushiriki kwenye Tovuti ya Wikimedia bila sisi kujua. Sera hii haidhibiti jinsi watu wengine wanavyoshughulikia maelezo wanayopokea kutoka kwa zana kama hiyo. Ukiona zana kama hiyo ya watu wengine, na unaamini inakiuka Sera hii, unaweza kuiondoa mwenyewe, au uripoti kwa kutuma ujumbe kwa privacywikimedia.org ili tukuchunguze.