Policy:Privacy policy/Definitions/sw

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
This page is a translated version of the page Policy:Privacy policy/Definitions and the translation is 90% complete.

Wikimedia Foundation Privacy Policy Definitions

Tukisema... ...tunaamini:
"Wakfu wa Wikimedia" / "Wakfu" / "sisi" / "yetu" Wikimedia Foundation, Inc., shirika lisilo la faida linaloendesha Tovuti za Wikimedia.
"Tovuti za Wikimedia" / "huduma zetu" Tovuti na huduma za Wikimedia (licha ya lugha zake), pamoja na miradi yetu mikuu, kama vile Wikipedia na Wikimedia Commons, pamoja na programu za simu, Violesura vya Usanidi wa Programu (API), barua pepe, na arifa; ukiondoa, hata hivyo, tovuti na huduma zilizoorodheshwa katika sehemu ya "Vipengele Ambavyo Havipo Chini ya Sera hii ya Faragha" hapa chini.
"wewe" / "yako" / "mimi" Wewe, licha ya kuwa wewe ni mtu binafsi, kundi au shirika, na licha ya kuwa unatumia Tovuti za Wikimedia au huduma zetu kwa niaba yako mwenyewe au ya mtu mwingine.
"Sera hii" / "Sera hii ya Faragha" Hati hii, yenye jina "Sera ya Faragha ya Wakfu wa Wikimedia".
"michango" Maudhui unayoweka au mabadiliko unayofanya kwenye sehemu yoyote ya Tovuti za Wikimedia.
"Maelezo ya Kibinafsi" Maelezo unayotupatia au maelezo tunayokusanya ambayo yanaweza kutumika kukutambulisha kibinafsi. Kumbuka, ingawa hatukusanyi aina zote za maelezo zifuatazo, tunazingatia angalau aina zifuatazo kuwa "maelezo ya kibinafsi" ikiwa si ya hadharani na yanaweza kutumiwa kukutambulisha:
(a) jina lako halisi, anwani, nambari ya simu, anwani ya barua pepe, nenosiri, nambari ya kitambulisho cha kitaifa, anwani ya IP, maelezo ya mtumiaji au wakala, nambari ya akaunti ya malipo;
(b) ikihusishwa na mojawapo ya vipengele vilivyo kwenye kifungu kidogo cha (a), maelezo yoyote nyeti kama vile tarehe ya kuzaliwa, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, asili ya rangi au kabila, hali ya ndoa au familia, hali ya matibabu au ulemavu, mwelekeo wa kisiasa na dini.
"mtu mwingine" / "watu wengine" Watu binafsi, vyombo, tovuti, huduma, bidhaa na programu ambazo hazidhibitiwi, kusimamiwa, au kuendeshwa na Wakfu wa Wikimedia. Hii ni pamoja na watumiaji wengine wa Wikimedia na mashirika au vikundi huru vinavyosaidia kukuza shughuli za Wikimedia kama vile tanzu za Wikimedia, mashirika yanayotekeleza mada maalum, na makundi ya watumiaji pamoja na watu wa kujitolea, wafanyakazi, wakurugenzi, maafisa, wapokeaji ruzuku, na makandarasi wa mashirika au vikundi hivyo.
Privacy-related pages