Policy:Privacy policy/Summary/sw
Appearance
Want to help translate? Translate the missing messages.
Sera ya Faragha
This is a summary of the Privacy Policy. To read the full terms, click here.
Kanusho: Muhtasari huu si sehemu ya Sera ya Faragha na si hati ya kisheria. Ni rejeleo la karibu la kuelewa Sera kamili ya Faragha. Lichukulie kuwa kiolesura bora cha Sera yetu ya Faragha.
Kwa sababu tunaamini kwamba hupaswi kutoa taarifa binafsi ili ushiriki katika vuguvugu la maarifa huru, unaweza:
- Soma, hariri, au tumia Tovuti yoyote ya Wikimedia bila kusajili akaunti.
- Jisajili kwa akaunti bila kutoa anwani ya barua pepe wala jina kamili.
Kwa sababu tunataka uelewe jinsi Tovuti za Wikimedia zinavyotumiwa ili tuziboreshe kwa ajili yako, tunakusanya baadhi ya taarifa wakati:
- Kutoa michango hadharani.
- Kusajili akaunti au kusasisha ukurasa wako wa mtumiaji.
- Kutumia Tovuti za Wikimedia.
- Kututumia barua pepe au kushiriki katika utafiti au kutoa maoni.
Tumeahidi:
- Kueleza jinsi taarifa zako zinavyoweza kutumika au kushirikiwa katika Sera hii ya Faragha.
- Kutumia hatua mwafaka kudumisha usalama wa maelezo yako.
- Kutouza maelezo yako kamwe au kuyashiriki na watu wengine kwa madhumuni ya utangazaji wa mauzo.
- Kushiriki maelezo yako tu katika hali chache maalum, kama vile ili kuboresha Tovuti za Wikimedia, kutii sheria, au kukulinda wewe na watu wengine.
- Kuhifadhi maelezo yako kwa muda mfupi zaidi iwezekanavyo unaolingana na malengo ya kuendesha, kuelewa na kuboresha Tovuti za Wikimedia, na majukumu yetu chini ya sheria inayotumika.
Jihadhari:
- Maudhui yoyote unayoongeza au mabadiliko yoyote unayofanya kwenye Tovuti ya Wikimedia yataweza kupatikana kwa uma na wakati wote.
- Ukiongeza maudhui au kufanya mabadiliko kwenye Tovuti ya Wikimedia bila kuingia, maudhui au mabadiliko hayo yatahusishwa hadharani na kwa wakati wote kwenye anwani ya IP iliyotumiwa wakati huo, badala ya jina la mtumiaji.
- Jamii yetu ya wahariri wa kujitolea na wachangiaji ni kikosi kinachojidhibiti chenyewe. Wasimamizi fulani wa Tovuti za Wikimedia, ambao huchaguliwa na jamii hutumia zana zinazowapa ufikiaji mdogo wa maelezo yasiyo ya umma kuhusu michango ya hivi majuzi ili waweze kulinda Tovuti za Wikimedia na kutekeleza sera.
- Sera hii ya Faragha haitumiki kwa tovuti na huduma zote zinazoendeshwa na Wakfu ya Wikimedia, kama vile tovuti au huduma zilizo na sera zake za faragha (kama vile Duka la Wikimedia) au tovuti au huduma zinazoendeshwa na watu wengine (kama miradi ya wasanidi programu wengine kwenye Huduma za Wingu za Wikimedia).
- Kama sehemu ya juhudi zetu za kutoa elimu na kufanya utafiti kote ulimwenguni, mara kwa mara tunatoa maelezo kwa umma na maelezo ya jumla au yasiyo ya kibinafsi kwa umma kupitia mafungu ya data na seti za data.
- Ili kulinda Wakfu wa Wikimedia na watumiaji wengine, ikiwa hukubaliani na Sera hii ya Faragha, unaweza kukosa kutumia Tovuti za Wikimedia.