Kanuni Majumui za Maadili/Miongozo ya Utekelezaji

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
This page is a translated version of the page Policy:Universal Code of Conduct/Enforcement guidelines and the translation is 98% complete.
Outdated translations are marked like this.
Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili wa Shirika la Wikimedia

1. Miongozo ya Utekelezaji wa UCoC

Miongozo hii ya Utekelezaji inaelezea jinsi jumuiya na Wikimedia Foundation wataweza kufikia malengo ya Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (UCoC). Hii ni pamoja na, miongoni mwa mada nyingine: kukuza uelewa wa UCoC, kushiriki katika kazi ya haraka ili kuzuia ukiukaji, kubuni kanuni za kushughulikia ukiukaji wa UCoC, na kusaidia miundo ya utekelezaji wa ndani.

UCoC inatumika kwa nafasi zote za mtandaoni na nje ya mtandao wa Wikimedia. Kwa hivyo, kutekeleza UCoC ni jukumu la Pamoja. Sambamba na kanuni ya harakati ya ugatuaji, UCoC inapaswa kutekelezwa katika ngazi ya ndani iwezekanavyo.

Miongozo ya Utekelezaji hutoa mfumo wa mwingiliano wa miundo ya sasa na ya baadaye ya utekelezaji, ikitafuta kuunda msingi wa utekelezaji sawa na Thabiti wa UCoC.

1.1 Tafsiri za Miongozo ya Utekelezaji ya UCoC

Toleo la asili la Miongozo ya Utekelezaji ya UCoC ni kwa Kiingereza. Itatafsiriwa kwa lugha mbalimbali zinazotumiwa kwenye miradi ya Wikimedia. Wikimedia Foundation itafanya juhudi zake zote ili kuwa na tafsiri sahihi. Ikiwa tofauti yoyote itajitokeza katika maana kati ya toleo la Kiingereza na tafsiri, maamuzi yatatokana na toleo la Kiingereza.

1.2 Ukaguzi wa Miongozo ya Utekelezaji ya UCoC

Kulingana na pendekezo la Bodi ya Wadhamini, mwaka mmoja baada ya kuidhinishwa kwa Miongozo ya Utekelezaji, Wikimedia Foundation itaandaa mashauriano ya jamii na ukaguzi wa Miongozo ya Utekelezaji ya UCoC na UCoC.

2. Kazi ya kuzuia

Sehemu hii inalenga kutoa miongozo kwa jumuiya za Wikimedia na washirika binafsi kufahamu UCoC, kuielewa kikamilifu na kuizingatia. Kwa ajili hiyo, sehemu hii itaeleza kwa kina mapendekezo ya kuongeza ufahamu kuhusu UCoC, kushughulikia tafsiri za UCoC, na kukuza ufuasi wa hiari kwa UCoC inapofaa au inapobidi.

2.1 Taarifa na uthibitisho wa UCoC

UCoC inatumika kwa kila mtu anayeshiriki na kuchangia kwenye miradi ya Wikimedia. Pia inatumika kwa matukio rasmi ya ana kwa ana, na nafasi zinazohusiana zinazopangishwa kwenye mifumo ya wahusika wengine kama msingi wa tabia ya ushirikiano kwenye miradi ya Wikimedia duniani kote.

Tunapendekeza UCoC iongezwe kwenye Masharti ya Matumizi ya Wikimedia.

Zaidi ya hayo, watu wafuatao wanahitajika kuthibitisha ufuasi wao kwa UCoC:

  • Wafanyakazi na makontrakta wote wa Wikimedia Foundation, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, wajumbe wa bodi ya washirika ya Wikimedia na wafanyakazi;
  • Mwakilishi yeyote wa mshirika wa Wikimedia au mshirika wa Wikimedia anayetaka (kama vile, lakini bila ukomo wa: mtu binafsi, au kikundi cha watu wanaotafuta kukuza na/au kushirikiana katika tukio la Wikimedia lililofadhiliwa, kikundi, uchunguzi, ama kwenye au nje ya wiki katika mazingira ya utafiti); na
  • Mtu yeyote anayetaka kutumia alama ya biashara ya Wikimedia Foundation katika tukio kama vile, lakini bila ukomo wa: matukio yaliyo na alama ya biashara za Wikimedia (kama vile kwa kuwajumuisha katika kichwa cha tukio) na uwasilishi wa shirika la Wikimedia, jumuiya, ao miradi katika tukio (kama vile, lakini bila kukomea kwa, mtangazaji au mwendeshaji wa kibanda).

2.1.1 Kukuza ufahamu wa UCoC

Ili kukuza ufahamu, kiungo cha UCoC kitapatikana kwenye au katika:

  • Kurasa za usajili wa mtumiaji na tukio;
  • Vijachini kwenye miradi ya Wikimedia na kurasa za uthibitishaji wa uhariri kwa watumiaji waliotoka (inapofaa na kitaalamu kuwezekana);
  • Vijachini kwenye tovuti za washirika wanatambulika na vikujndi vya watumiaji;
  • Kuwasiliana kwa uwazi katika matukio ya ana kwa ana, ya mbali na ya mseto; na
  • Mahali popote panapoonekana kufaa na miradi ya ndani, washirika, vikundi vya watumiaji na waratibu wa hafla.

2.2 Mapendekezo ya mafunzo ya UCoC

Kamati ya Ujenzi ya U4C, kwa msaada wa Wikimedia Foundation, itakuza na kutekeleza mafunzo ili kutoa uelewa wa pamoja wa UCoC na ujuzi wa utekelezaji wake. Inapendekezwa kuwa wadau husika wanapaswa kushauriwa katika uandaaji wa mafunzo, ikijumuisha, lakini sio tu kwa: Washirika, Kamati ya Ushirikiano, Kamati za Usuluhishi, Wasimamizi na Wamiliki wengine wa Haki za Juu, T&S na kisheria, na wengine kama inavyoonekana kuwa na manufaa kwa kutoa mtazamo kamili wa UCoC.

Mafunzo haya yanalenga watu wanaotaka kuwa sehemu ya michakato ya utekelezaji wa UCoC, au wale wanaotaka kufahamishwa kuhusu UCoC.

Mafunzo yatawekwa katika moduli za kujitegemea zinazojumuisha habari za jumla, utambuzi wa ukiukaji na usaidizi, na kesi ngumu na rufaa. Baada ya U4C ya kwanza kuingizwa, itakuwa na jukumu la kudumisha na kusasisha moduli za mafunzo inapohitajika.

Moduli za mafunzo zitapatikana katika miundo tofauti na kwenye majukwaa tofauti kwa ufikiaji rahisi. Jumuiya za wenyeji na Washirika wa Wikimedia wanaotaka kutoa mafunzo katika ngazi ya jumuiya yao watapata usaidizi wa kifedha kutoka kwa Wikimedia Foundation ili kutekeleza mafunzo. Hii inajumuisha usaidizi wa tafsiri.

Tunapendekeza washiriki wanaokamilisha moduli wanapaswa kuwa na chaguo la ukamilishaji wao kutambuliwa hadharani.

Seti zifuatazo za mafunzo zinapendekezwa:

Moduli A - Mwelekeo (UCoC - Jumla)

  • Itasaidia kuhakikisha uelewa wa pamoja wa UCoC na utekelezaji wake
  • Inaeleza kwa ufupi UCoC ni nini na ni aina gani ya utekelezaji utakaotarajiwa, pamoja na zana zipi zinazopatikana kuripoti ukiukaji.

Moduli B - Utambulisho na Kuripoti (UCoC - Ukiukwaji)

  • Inawapa watu uwezo wa kutambua ukiukwaji wa UCoC, kuelewa michakato ya kuripoti na kujifunza jinsi ya kutumia zana.
  • Inaeleza Zaidi aina ya ukiukwaji, jinsi ya kutambua matukio yanayoweza kuripotiwa katika muktadha wa eneo lao, jinsi na mahali pa kutoa ripoti, na ushughulikiaji bora wa kesi ndani ya michakato ya UCoC.
  • Mafunzo pia yatalenga sehemu mahususi za UCoC, kama vile unyanyasaji na matumizi mabaya ya mamlaka.

Moduli C - Kesi changamano, Rufaa (UCoC - Ukiukwaji Mwingi, Rufaa)

  • Moduli hizi ni sharti la kujiunga na U4C, na zinapendekezwa kwa waombaji watarajiwa wa U4C na wenye haki za juu.
  • Moduli hii inapaswa kushughulikia mada mbili maalumu:
    • C1- Kushughulikia kesi changamano (UCoC - Ukiukwaji Mwingi): Kushughulikia kesi mbalimbali za wiki, unyanyasanyi wa muda mrefu, kutambua uaminifu wa vitisho, mawasiliano madhubuti na nyeti, na kulinda usalama wa wahasiriwa na watu wengine walio hatarini.
    • C2 - Kushughulikia rufaa, kufunga kesi (UCoC - Rufaa): Ushughulikiaji wa rufaa za UCoC.
  • Moduli hizi zitakuwa mafunzo yanayoongozwa na wakufunzi na yaliyolengwa, yatatolewa kwa wanachama na waombaji wa U4C, na watendaji waliochaguliwa na jamii ambao wametia saini Upataji wa Sera ya Data ya kibinafsi Isiyo ya Umma
  • Inapowezekana nyenzo za mafunzo haya yanaoongozwa na wakufunzi, kama vile moduli za kibinafsi, slaidi, maswali,n.k. zitapatikana kwa umma

3. Kazi ya kujibu

Sehemu hii inalenga kutoa miongozo na kanuni za kuchakata ripoti za ukiukwaji wa UCoC, na mapendekezo ya miundo ya utekelezaji ya ndani inayoshughulikia ukiukwaji wa UCoC. Kwa ajili hiyo, sehemu hii itaeleza kwa kina kanuni muhimu za kuchakata ripoti, mapendekezo ya kuundwa kwa zana ya kuripoti, mapendekezo ya utekelezaji wa viwango tofauti vya ukiukaji na mapendekezo ya miundo ya utekelezaji wa ndani.

3.1 Kanuni za kufungua jalada na kuchakata ukiukaji wa UCoC

Kanuni zifuatazo ni viwango vya mifumo ya kuripoti kote Katika Harakati.

Ripoti:

  • Kuripoti ukiukwaji wa UCoC kunapaswa kuwezekana kwa lengo la ukiukaji huo, na vile vile watu wengine ambao hawakuhusika walioona tukio hilo.
  • Ripoti zitakuwa na uwezo wa kuangazia ukiukwaji wa UCoC, uwe unafanyika mtandaoni, nje ya mtandao, Katika nafasi inayopangishwa na wahusika wengine au mchanganyiko wa nafasi.
  • Ni lazima iwezekane kwa ripoti kufanywa hadharani au kwa viwango tofauti vya faragha.
  • Uaminifu na uthibitisho wa shutuma utachunguzwa kwa kina ili kutathmini ipasavyo hatari na uhalali.
  • Watumiaji ambao mara kwa mara wanatuma imani mbaya au ripoti zisizo na uhalali huhatarisha kupoteza haki za kuripoti.
  • Watu wanaoshutumiwa wataweza kupata maelezo ya madai ya ukiuakaji ulifanywa dhidi yao isipokuwa kama ufikiaji huo utaleta hatari au madhara kwa mwandishi au usalama wa watu wengine.
  • Rasilimali za kutafsiri lazima zitolewe na Wikimedia Foundation wakati ripoti zinatolewa katika lugha ambazo watu walioteuliwa watu walioteuliwa hawana ujuzi.

Uchakataji wa ukiukwaji:

  • Matokeo yatakuwa sawia na ukali wa ukiukaji
  • Kesi zitahukumiwa kwa njia ya ufahamu, ambayo inatumia muktadha, kwa kuzingatia kanuni za UCoC.
  • Kesi zitasuruhishwa ndani ya muda maalumu, na masasisho yakitolewa kwa wakati kwa washiriki ikiwa utarefushwa.

Uwazi:

  • Inapowezekana, kikundi kilichoshughulikia ukiukwaji wa UCoC kitatoa kumbukumbu ya umma ya kesi hizo, huku kikihifadhi faragha na usalama katika kesi zisizo za umma.
  • Wikimedia Foundation itachapisha takwimu za kimsingi kuhusu matumizi ya zana kuu ya kuripoti iliyopendekezwa katika sehemu ya 3.2, huku ikiheshimu kanuni za ukusanyaji mdogo wa data na kuheshimu faragha.
    • Vikundi vingine vinavyoshughulikia ukiukwaji wa UCoC vinahimizwa kutoa takwimu za kimsingi kuhusu ukiukwaji wa UCoC na kuripoti kadri wanavyoweza, huku wakiheshimu kanuni za ukusanyaji mdogo wa data na kuheshimu faragha.

3.1.1 Kutoa rasilimali za kuchakata kesi

Utekelezaji wa UCoC na miundo ya utawala wa ndani utasaidiwa kwa njia nyingi. Jamii zitaweza kuchagua kutoka kwa mifumo au mbinu tofauti kulingana na mambo kadhaa kama vile: uwezo wa miundo ya utekelezaji, mtazamo wa utawala, na mapendeleo ya jamii. Baadhi ya mbinu hizi zinaweza kujumuisha:

  • Kamati ya Usuluhishi (ArbCom) kwa mradi mahususi wa Wikimedia
  • ArbCom iliyoshirikiwa miongoni mwa miradi mingi ya Wikimedia
  • Wenye haki za juu wanaotekeleza sera za ndani zinazowiana na UCoC kwa njia ya ukatuzi
  • Majopo ya wasimamizi wa ndani wanaotekeleza sera
  • Wachangiaji wa ndani wanaotekeleza sera za ndani kupitia majadiliano na makubaliano ya jumuiya

Jumuiya zinapaswa kuendelea kushughulikia utekelezaji kupitia njia zilizopo ambapo hazihitilafiwi na UCoC.

3.1.2 Utekelezaji kwa aina ya ukiukwaji

Sehemu hii inaeleza orodha isiyo kamili ya aina tofauti za ukiukwaji, pamoja na uwezekano wa utaratibu wa utekelezaji unaohusiana nao.

  • Ukiukwaji unahusisha vitisho vya aina yoyote ya unyanyasaji wa kimwili
    • Inashughulikiwa na timu ya Imani na Usalama ya Wikimedia
  • Ukiukaji unahusisha madai au vitisho vya kisheria
    • Imetumwa kwa timu ya Kisheria ya Wikimedia Foundation, au, inapofaa, wataalamu wengine ambao wanaweza kutathmini ipasavyo manufaa ya vitisho.
  • Ukiukaji unaohusisha ufichuaji bila kibali cha maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu binafsi
    • Kwa ujumla hushughulikiwa na watumiaji walio na uangalizi au ruhusa za ukandamizaji.
    • Hushughulikiwa mara kwa mara na Imani na Usalama
    • Imetumwa kwa timu ya Kisheria ya Wikimedia Foundation au, inapofaa, wataalamu wengine ambao wanaweza kutathmini ipasavyo manufaa ya kesi ikiwa ukiukaji wa aina hii unatoa wajibu wa kisheria.
  • Ukiukwaji unaohusiana na utawala wa washirika
  • Inashughulikiwa na Kamati ya Ushirikiano au chombo sawa
  • Ukiukwaji katika nafasi za kiufundi
  • Inashughulikiwa na Kamati ya Maadili ya Kiufundi
  • Kushindwa kimfumo kufuata UCoC
    • Inashughulikiwa na U4C
    • Baadhi ya mifano ya kushindwa kimfumo ni pamoja na:
      • Ukosefu wa uwezo wa ndani wa kutekeleza UCoC
      • Maamuzi ya ndani ambayo yanakinzana na UCoC
      • Kukataa kutekeleza UCoC
      • Ukosefu wa rasilimali au ukosefu wa nia ya kushughulikia masuala
  • Ukiukaji wa wiki kwenye U4C
      • Ukiukwaji wa UCoC unaotokea kwenye Wiki nyingi: Hushughulikiwa na wasimamizi wa kimataifa na mashirika ambayo hushughulikia ukiukwaji wa UCoC wa Wiki moja au kushughulikiwa na U4C ambapo haipingani na miongozo hii.
      • Ukiukwaji wa UCoC unaotokea kwenye wiki moja: Unashughulikiwa na miundo iliyopo ya utekelezaji kulingana na miongozo yao iliyopo, ambapo haipingani na miongozo hii.
      • Ukiukwaji rahisi wa UCoC kama vile uharibifu unapaswa kushughulikiwa na miundo iliyopo ya utekelezaji kupitia njia zilizopo, ambapo haipingani na miongozo hii.
  • Ukiukwaji Katika nafasi za kiufundi
    • Inashughulikiwa na Kamati ya Maadili ya Kiufundi
  • Ukiukwaji wa nje ya wiki
    • Inashughulikiwa na U4C ambapo hakuna muundo wa utawala wa ndani (km. ArbCom) uliopo, au ikiwa kesi itatumwa kwao na muundo wa utekelezaji ambao ungewajibijika kwao.
    • Katika baadhi ya matukio, inaweza saidia kuripoti ukiukwaji wa nje ya wiki kwa miundo ya utekelezaji ya nafasi husika ya nje ya wiki. Hii haizuii mifumo iliyopo ya utekelezaji wa ndani na kimataifa kutekeleza ripoti
  • Ukiukwaji katika matukio kibinafsi na nafasi
    • Miundo iliyopo ya utekelezaji mara nyingi hutoa sheria za tabia na utekelezaji katika nafasi zisizo za wiki. Hizi ni pamoja na sera za anga za kirafiki na sheria za matukio
    • Miundo ya utekelezaji inayoshughulikia kesi hizi inaweza kuzielekeza kwa U4C
    • Katika mifano ya matukio yanayoandaliwa na Wikimedia Foundation, Imani na Usalama hutoa hutoa utekelezaji wa sera.

3.2 Mapendekezo ya zana ya kuripoti

Chombo cha kati cha kuripoti na kuchakata ukiukwaji wa UCoC kitaundwa na kudumishwa na Wikimedia Foundation. Itawezekana kutoa ripoti kupitia MediWiki kwa hii zana. Madhumuni ni kupunguza kizuizi cha kiufundi cha kuripoti na kushughulikia ukiukwaji wa UCoC.

Ripoti zinapaswa kujumuisha taarifa muhimu zinazoweza kuchukuliwa hatua au kutoa rekodi ya hati ya kesi iliyopo. Kikusa cha kuripoti kinapaswa kumruhusu mwandishi kutoa maelezo kwa yeyote anayehusika na kushulikia kesi hiyo mahususi. Hii inajumuisha habari kama vile, lakini sio tu kwa:

  • Jinsi tabia iliyoripotiwa inakiuka UCoC
  • Nani au nini kimeumizwa na ukiukaji huu wa UCoC
  • Tarehe na wakati tukio ambapo tukio hilo, lilitokea
  • Mahali pa tukio (ma)
  • Taarifa nyingine ili kuruhusu vikundi vya utekelezaji kushughulikia suala hilo vyema.

Zana inapaswa kufanya kazi chini ya kanuni za urahisi wa kutumia, faragha na usalama, kubadilika katika kuchakata, na uwazi.

Watu waliopewa wajibu wa kutekeleza UCoC hawahitajiki kutumia zana hii. Wanaweza kuendelea kufanya kazi na zana zozote wanazoona zinafaa, ilimradi kesi zinashughulikiwa kulingana na kanuni sawa za urahisi wa utumiaji, faragha na usalama, kubadilika katika kuchakata na uwazi.

3.3 Kanuni na miundo ya mapendekezo ya miundo ya utekelezaji

Inapowezekana, tunahimiza miundo iliyopo ya utekelezaji kuchukua jukumu la kupokea ripoti za na kushughulikia ukiukwaji wa UCoC, kwa mujibu wa miongozo iliyotajwa hapa. Ili kuhakikisha kwamba utekelezaji wa UCoC unasalia thabiti katika harakati zote, tunapendekeza kwamba kanuni za msingi zifuatazo zitumike wakati wa kushughulikia ukiukwaji wa UCoC.

3.3.1 Haki Katika mchakato

Tunahimiza miundo ya utekelezaji katika kuunda na kudumisha sera zinazounga mkono migogoro ya maslahi. Hizi zinapaswa kuwasaidia wasimamizi au watu wengine kubaini wakati wa kujiepusha au kuondokana na ripoti wakati wanahusika kwa karibu katika suala hilo.

Wahusika wote kwa kawaida watapata fursa ya kutoa mtazamo wao kuhusu hayo masuala na Ushahidi, na maoni kutoka kwa wengine yanaweza pia kukaribishwa ili kusaidia kutoa maelezo zaidi, mtazamo na muktadha. Hii inaweza kuzuiwa ili kulinda faragha na usalama.

3.3.2 Uwazi wa mchakato

U4C, kulingana na madhumuni na upeo wake kama inavyofafanuliwa Katika 4.1, itatoa hati kuhusu ufanisi wa vitendo vya kutekeleza UCoC na uhusiano wao na ukiukwaji wa kawaida katika harakati zote. Wanapaswa kuungwa mkono na Wikimedia Foundation katika kufanya utafiti huu. Lengo la hati hii ni kusaidia miundo ya utekelezaji katika kubuni mbinu bora za kutekeleza UCoC.

Miradi ya Wikimedia na washirika, inapowezekana, watadumisha kurasa zinazoelezea sera na mifumo ya utekelezaji kulingana na maandishi ya sera ya UCoC. Miradi na washirika pamoja na miongozo au sera zilizopo kinyume na maandishi ya sera ya UCoC wanapaswa kujadili mabadiliko ili kuendana na viwango vya kimataifa. Kusasisha au kuunda sera mpya za ndani kunapaswa kufanywa kwa njia ambayo haipingani na UCoC. Miradi na washirika wanaweza kuomba maoni ya ushauri kutoka kwa E4C kuhusu uwezekano wa sera au miongozo mipya.

Kwa mazungumzo mahususi ya Wikimedia yanayotokea kwenye nafasi inayohusiana iliyopangishwa kwenye mifumo ya watu wengine (k.m. Discord, Telegram, n.k), Masharti ya Matumizi ya Wikimedia huenda yasitumike. Zinasimamiwa na Masharti ya Matumizi na sera za mwenendo za tovuti hiyo. Hata hivyo, tabia za Wanawikimedia kwenye nafasi inayohusiana iliyopangishwa kwenye mifumo ya wahusika weingine inaweza kukubalika kama ushahidi Katika ripoti za ukiukwaji wa UCoC. Tunawahimiza wanajamii wa Wikimedia wanaosimamia nafasi zinazohusiana na Wikimedia kwenye mifumo ya wahusika wengine kujumuisha heshima ya UCoC Katika sera zao Wikimedia Foundation inapaswa kutafuta kuhimiza mbinu bora za mifumo ya watu wengine ambayo inakatisha tamaa kuendelea kwa mizozo katika nafasi zao.

3.3.3 Rufaa

Hatua iliyochukuliwa na mwenye haki za juu itaweza kukatiwa rufaa kwa muundo wa ndani au wa pamoja wa utekelezaji isipokuwa U4C. Ikiwa hakuna muundo kama huo wa utekelezaji, basi rufaa kwa U4C inaweza kuruhusiwa. Kando na mpangilio huu, jumuiya za wenyeji zinaweza kuruhusu rufaa kwa mtu tofauti mwenye haki za juu.

Miundo ya utekelezaji itaweka viwango vya kukubali na kuzingatia rufaa kulingana na maelezo muhimu ya muktadha na sababu za kupunguza. Sababu hizi ni pamoja na, lakini sio tu: uthibitishaji wa mashtaka, urefu na athari ya vikwazo, na kama kuna shaka ya matumizi mabaya ya mamlaka au masuala mengine ya kimfumo, na uwezekano wa ukiukwaji zaidi. Kukubaliwa kwa rufaa hakuhakikishiwa.

Rufaa haiwezekani dhidi ya maamuzi fulani yaliyotolewa na idara ya Sheria ya Wikimedia Foundation. Hata hivyo, baadhi ya hatua na maamuzi ya ofisi ya Wikimedia Foundation yanaweza kukaguliwa na Kamati ya Kupitia Kesi. Kizuizi, haswa kuhusu rufaa kutoka kwa vitendo na maamuzi ya ofisi, huenda kisitumike katika baadhi ya maeneo ya mamlaka, ikiwa mahitaji ya kisheria yatatofautiana.

Miundo ya utekelezaji inapaswa kutafuta mitizamo iliyoarifiwa kuhusu kesi ili kuweka msingi wa kukubali au kukataa rufaa. Taarifa inafaa kushughulikiwa kwa uangalifu, kwa kujali usiri wa watu wanaohusika na mchakato wa kufanya maamuzi.

Ili kufikia lengo hili tunapendekeza kwamba miundo ya utekelezaji inapaswa kuzingatia vipengele tofauti wakati wa kupitia rufaa. Hizi zinaweza kujumuisha, lakini zisizuiliwe kwa:

  • Ukali na madhara yanayosababishwana ukiukwaji
  • Historia ya awali ya ukiukwaji
  • Ukali wa vikwazo uliokatiwa rufaa
  • Urefu wa muda tangu ukiukaji
  • Uchambuzi wa ukiukwaji katika kuwasiliana
  • Tuhuma za uwezekano wa matumizi mabaya ya madaraka au suala lingine la kimfumo

4. Kamati ya Uratibu ya UCoC (U4C)

Kamati mpya ya kimataifa inayoitwa Kamati ya Kuratibu Kanuni Majumui za Maadili (U4C) itaundwa. Kamati hii itakuwa chombo chenye usawa na vyombo vingine vya juu vya kufanya maamuzi (k.m. ArbComs na AffCom). Madhumuni yake ni kutumika kama njia ya mwisho katika kesi ya kushindwa kwa mfumo na vikundi ya ndani kutekeleza UCoC. Uanachama wa U4C utaakisi muundo wa jumuiya na utofauti wa jumuiya yetu ya kimataifa.

4.1 Kusudi na upeo

U4C hufuatilia ripoti za ukiukaji wa UCoC, na inaweza kufanya uchunguzi wa ziada na kuchukua hatua inapofaa. U4C inafuatilia na kutathmini mara kwa mara hali ya utekelezaji wa UCoC. Inaweza kupendekeza mabadiliko yanayofaa kwa UCoC na Mwongozo wa Utekelezaji wa UCoC kwa Wikimedia na jumuiya kwa kuzingatia, lakini haiwezi kubadilisha hati yoyote yenyewe. Inapobidi U4C itasaidia Wikimedia Foundation katika kushughulikia kesi.

U4C:

  • Hushughulikia malalamiko na rufaa katika hali zilizoanishwa katika Miongozo ya Utekelezaji.
  • Hufanya uchunguzi wowote muhimu ili kutatua malalamiko na rufaa zilizotajwa
  • Inatoa nyenzo kwa jumuiya kuhusu mbinu bora za U4C, kama vile nyenzo za lazima za mafunzo na nyenzo zinginezo kama zinahitajika
  • Hutoa tafsiri ya mwisho ya Miongozo ya Utekelezaji ya UCoC na UCoC ikiwa hitaji litatokea, kwa ushirikiano na wanajamii na miundo ya utekelezaji.
  • Inafuatilia na kutathmini ufanisi wa utekelezaji wa UCoC, na hutoa mapendekezo ya kuboresha.

U4C haitachukua kesi ambazo hazihusishi na ukiukwaji wa CoC, U4C inaweza kukabidhi mamlaka yake yote ya kufanya maamuzi isipokuwa katika hali ya masuala mazito ya kimfumo. Majukumu ya E4U yanaelezwa katika muktadha ya miundo mingine ya utekelezaji katika 3.1.2.

4.2 Uteuzi, uanachama na majukumu

Uchaguzi wa kila mwaka, unaoandaliwa na jamii ya kimataifa kwa usaidizi kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika inapohitajika, utachagua washiriki wa kupiga kura. Wagombea wanaweza kuwa mwanajamii ambaye lazima pia:

  • Fikia vigezo vya Wikimedia Foundation vya kufikia data ya kibinafsi isiyo ya umma na wathibitishe katika taarifa yao ya uchaguzi kuwa watatii vigezo kikamilifu.
  • Kwa sasa hana adhabu katika mradi wowote wa Wikimedia au kuwa na marufuku ya tukio
  • Kuzingatia UCoC
  • Kukidhi mahitaji mengine yoyote ya ustahiki yaliyobainishwa wakati wa mchakato wa uchaguzi

Katika hali za kipekee, U4C inaweza kuitisha chaguzi za muda, ikiwa itabainisha kuwa kujiuzulu au kutoshiriki kumesababisha hitaji la haraka la wanachama zaidi. Chaguzi zitakuwa katika muundo sawa na ule wa chaguzi za kawaida za kila mwaka.

Wanachama binafsi wa U4C hawalazimiki kujiuzulu kutoka nyadhifa zingine (km. synop ya ndani, mwanachama wa ArbCom, mratibu wa usalama wa hafla). Hata hivyo wanaweza wasishiriki katika kushughulikia kesi ambazo wamehusika moja kwa moja kutokana na nyadhifa zao nyingine. Wanachama wa U4C watatia saini Sera ya Kufikia Data ya Kibinafsi Isiyo ya Umma ili kuwapa ufikiaji wa taarifa zisizo za umma. Kamati ya Ujenzi ya U4C inapaswa kuamua kuhusu masharti yanayofaa kwa wanachama wa U4C.

U4F inaweza kuunda kamati ndogo au kuteua watu binafsi kwa kazi au majukuu Fulani inavyofaa.

Wikimedia Foundation inaweza kuteua hadi wanachama wawili wasiopiga kura kwa U4C na itatoa wafanyakazi wa usaidizi kama inavyotakiwa na kufaa.

4.3 Taratibu

U4C itaamua ni mara ngapi itakutana na kuhusu taratibu zingine za uendeshaji. U4C inaweza kuunda au kurekebisha taratibu zao ilimradi tu ipo ndani ya mawanda yao. Inapobidi, Kamati inapaswa kukaribisha maoni ya jamii kuhusu mabadiliko yaliyokusudiwa kabla ya kuyatekeleza.

4.4 Sera na kigezo

U4C haiundi sera mpya na haiwezi kurekebisha au kubadilisha UCoC. U4C badala yake inatumika na kutekeleza UCoC kama inavyofafanuliwa na upeo wake.

Kadiri sera za jamii, miongozo na kanuni zinavyobadilika kwa wakati, maamuzi ya awali yatazingatiwa tu kwa kiwango ambacho yanabaki kuwa muhimu katika muktadha wa sasa.

4.5 Kamati ya Ujenzi ya U4C

Kufuatia kuthibitishwa kwa miongozo ya utekelezaji ya UCoC, Wikimedia Foundation itawezesha kamati ya Ujenzi ili:

  • Kubainisha taratibu, sera na matumizi ya vielelezo vya U4C
  • Kurasimu salio la mchakato wa U4C
  • Kuteua vifaa vingine vyovyote muhimu ili kuanzisha U4C
  • Kusaidia kuwezesha taratibu za awali za U4C

Kamati ya Ujenzi itajumuisha wanajamii wanaojitolea, wafanyakazi washirika au wajumbe wa bodi, na wafanyakazi wa Wikimedia Foundation.

Wanachama watachaguliwa na Makamu wa Rais wa Ustahimilivu wa Jamii na Uendelevu wa Wikimedia Foundation. Wanachama wa kujitolea wa kamati wanapaswa kuwa wanajamii wanaoheshimika.

Wanachama wataonyesha mitazamo mbalimbali ya michakato ya utekelezaji wa harakati wakiwa na uzoefu katika mambo kama vile, lakini sio tu: kuandaa sera, kuhusika na ufahamu wa matumizi ya sheria na sera zilizopo kwenye miradi ya Wikimedia, na kufanya maamuzi shirikishi. Wanachama wake wataakisi utofauti wa harakati, kama vile, lakini sio tu: lugha zinazozungumzwa, jinsia, umri, jiografia na aina ya mradi.

Kazi ya Kamati ya Ujenzi ya U4C itaidhinishwa na Baraza la Kimataifa au kwa mchakato wa jumuiya sawa na uidhinishaji wa hati hii. Kufuatia kuanzishwa kwa E4C kupitia kazi ya Kamati hii ya Ujenzi, Kamati ya ujenzi inapaswa kuvunjwa.

5. Faharasa

Msimamizi (sysop au admin)
Tazama ufafanuzi kwenye Meta.
Mwenye haki za juu
mtumiaji ambaye ana haki za usimamizi zaidi ya ruhusa za kawaida za uhariri, na kwa ujumla huchaguliwa kupitia michakato ya jumuiya au kuteuliwa na Kamati za Usuluhishi. Hii inajumuisha, kama orodha isiyo kamili: wasimamizi / wasimamizi wa ndani, watendaji, wasimamizi wa kimataifa, waandalizi.
Kamati ya Ushirikiano au Affcom
Tazama ufafanuzi kwenye Meta.

Kamati ya Usuluhishi au ArbCom: Kikundi cha watumiaji wanaoaminika ambao hutumika kama kikundi cha mwisho cha kufanya maamuzi kwa baadhi migogoro. Kila upeo wa ArbCom unafafanuliwa na jumuiya yake. ArbCom inaweza kutoa zaidi ya mradi mmoja (k.m Wikinews na Wikivoyage) na/au zaidi ya lugha moja. Kwa madhumuni ya miongozo hii, hii inajumuisha Kamati ya Kanuni za Maadili kwa Nafasi za Kiufundi za Wikimedia na paneli za usimamizi. Tazama pia ufafanuzi kwenye Meta.

Vitenzi vya kuunganisha

Wakati wa kuandaa Miongozo ya Utekelezaji, kamati ya uandishi ilizingatia maneno 'unda', 'kuza', 'tekeleza', 'lazima', 'kuza', 'itakuwa' na 'itafanya' kuwa ya lazima. Linganisha hii na vitenzi vya mapendekezo.

Kamati ya Uchunguzi wa Kesi

Tazama ufafanuzi kwenye Meta.

Jumuiya
Inahusu jamii ya mradi. Maamuzi yanayofanywa na jumuiya ya mradi kwa ujumla huuamuliwa kwa maafikiano. Tazama pia: Mradi.
Kuvuka-wiki
Kuathiri au kutokea kwenye Zaidi ya mradi mmoja. Tazama pia: Kimataifa.

Mratibu wa Usalama wa tukio: mtu aliyeteuliwa na waandaji wa tukio la ana kwa ana linalohusiana na Wikimedia kama mwajibikaji wa usalama na ulinzi wa tukio hilo.

Kimataifa
Ikimaanisha miradi yote Wikimedia. Katika harakati za Wikimedia, “kimataifa” ni neno la kitaalamu linalomaanisha mashirika ya utawala ya Harakati kote. Kwa ujumla hutumiwa kulinganisha dhidi ya “ndani”
Wasimamizi wa kimataifa
Tazama ufafanuzi kwenye Meta.
Bodi ya maamuzi ya kiwango cha juu
Kundi (yaani U4C, ArbCom, Affcom) zaidi ya hapo haliwezi kuwa na rufaa. Masuala tofauti yanaweza kuwa na vyombo tofauti ya kufanya maamuzi ya kiwango cha juu. Neno hili halijumuishi kundi la watumiaji wanashiriki katika majadiliano yaliyoandaliwa kwenye ubao wa matangazo na kusababisha uamuzi, hata kama matokeo ya majadiliano hayo hayawezi kukatiwa rufaa.
Ndani
Ikimaanisha mradi mradi mmoja wa Wikimedia, mshirika, au shirika. Neno hili kwa kawaida linamaanisha bodi tawala ndogo zaidi, ya haraka inayotumika kwa hali hiyo.
Nje ya wiki
Kwa ujumla inamaanisha nafasi za mtandaoni ambazo hazijapangishwa na Wikimedia hata kama wanajamii wapo na wanatumia nafasi hiyo kikamilifu. Mifano ya nafasi zisizo za wiki ni pamoja na Twitter, WhatsApp, IRC, Telegram, Discord, na Nyinginezo.
Taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu binafsi
ni data yoyote ambayo inayoweza kumtambulisha mtu mahususi. Taarifa yoyote ambayo inaweza kutumika kutofautisha mtu mmoja na mwingine na inaweza kutumika kuondoa utambulisho wa data isiyojulikana hapo awali inachukuliwa kama PII.
Mradi (mradi wa Wikimedia )
Wiki inayoendeshwa na WMF.
Vitenzi vya mapendekezo
Wakati wa kuandaa Miongozo ya Utekelezaji, kamati ya kuandaa ilizingatia maneno ‘himiza’, ‘naweza’, ‘pendekeza’, ‘pendekeza’ na ‘lazima’ kama mapendekezo. Linganisha hii na vitenzi vya kuunganisha.
Nafasi inayohusiana iliyopangishwa kwenye mifumo ya wahusika wengine
Tovuti ikijumuisha wiki za kibinafsi, zisizoendeswa na WMF lakini ambapo watumiaji hujadili mambo ya mradi yanayohusiana na Wikimedia. Mara nyingi husimamiwa na wafanyakazi wa kujitolea wa Wikimedia.
Wafanyakazi
Wafanyikazi wa na/au wafanyikazi waliopewa kazi ya shirika la harakati la Wikimedia au makontrakta wa shirika kama hilo la harakati ambao kazi yao inahitaji mwingiliano na wanajamii wa Wikimedia au katika nafasi za harakati za Wikimedia (pamoja na nafasi za watu wengine kama vile majukwaa ya nje ya Wiki yaliyotolewa kwa shughuli za harakati za Wikimedia. )
Msimamizi
Tazama ufafanuzi kwenye Meta.
Tatizo la kimfumo au kushindwa
Suala ambalo kuna mtindo wa kushindwa kufuata Kanuni Majumui za Maadili kwa kushirikisha watu kadhaa, hasa wale walio na haki za juu.
Sera ya Kitendo ya Ofisi ya Wikimedia Foundation

Sera inayopatikana kwenye Meta au sera sawa ya mrithi.